"Karibu katika Tovuti ya Bodi ya Mkonge Tanzania; Wewe ni wa thamani sana kwetu, asante kwa kutembelea tovuti yetu. Jiunge nasi ili ugundue singa asilia za Mkonge."
Shamba la mkonge wa Tanzania likiwa limepangwa kwa ustawi na uzalishaji endelevu.
Mashine ya kuchakata mkonge (dikotiketa) ni kifaa kinachotumika kuondoa nyama laini ya majani ya mkonge ili kubaki na nyuzi za mkonge zinazotumika kutengeneza kamba, mikeka, mazulia na bidhaa nyingine.
Marobota ya mkonge wa Tanzania yakipakuliwa bandarini kwa maandalizi ya safari ya kimataifa.
Marobota ya mkonge yakipakuliwa bandarini kwa maandalizi ya safari ya kimataifa
Marobota ya mkonge yakiwa yamehifadhiwa kwa mpangilio maalum ndani ya godauni.
Marobota ya mkonge yakiwa yamepakiwa kwenye kontena kwa maandalizi ya usafirishaji wa kimataifa.
Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano umeshiriki katika Mkutano wa Dunia wa Kutokomeza Utumikishwaji wa watoto uliofanyika nchini Morocco. TSB imewakilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Emmanuel Kimaro ( wa tatu kulia)
Menejimenti ya Bodi ya Mkonge Tanzania yakutana na kuzungumza na timu ya tathmini kutoka ofisi ya Msajili wa Hazina na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) wakati wa kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa Bodi kiichofanyika Mkonge House jijini Tanga.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) Saddy Kambona akizungumza na timu ya tathmini kutoka ofisi ya Msajili wa Hazina na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) wakati wa kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa Bodi kiichofanyika Mkonge House jijini Tanga.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania ( TSB) Saddy Kambona (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula ( NFRA) Dkt. Andrew Komba katika kikao kazi cha Wakuu wa Taasisi za Kilimo kilichofanyika Jijini Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Dkt. Batilida Burian akifurahia elimu ya kilimo Mseto cha Mkonge aliyopata katika banda la Bodi ya Mkonge Tanzania( TSB) wakati wa ziara yake ya kutembelea mabada ya maonesho katika ufunguzi wa maonesho ya Wiki ya Chakula Duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Biashara wa Kampuni inayojihusisha na biashara ya matrekta nchini (TAFE), Praveen Makala na Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni hiyo, Bosco Raj.
Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Mhe. Vu Thanh Huyen ametembelea Ofisi za Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) jijini Tanga kwa lengo la kujifunza kuhusu mnyororo mzima wa thamani wa zao la Mkonge
Ziara ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TSB katika mradi wa Mruazi Heifer Breaeding Unit ( HBU)
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TSB wakagua mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kuchakata Mkonge cha Taula kilichopo wilaya ya Handeni Mkoani Tanga
Waziri wa Kilimo, Mh. Hussein Bashe (wa pili kulia), akionyeshwa maeneo mbalimbali ya ofisi za Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) wakati akienda kuzindua Kituo Atamizi cha Mkonge BBT Tanga kinachosimamiwa na TSB.
Waziri wa Kilimo, Mh. Hussein Bashe (kulia) akipokea zawadi ya picha ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan iliyozalishwa kwa zao la Mkonge sanjari na bidhaa nyingine zinazotokana na zao hilo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mh. Japhari Kubecha.
Wakurugenzi TSB katika ziara
Mhe. Bashe azindua kituo atamizi cha Mkonge BBT
Wanajeshi kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi ( NDC) watembelea kitalu cha miche ya Mkonge TARI Mlingano, mkoani Tanga.