WAKURUGENZI TSB WAFANYA ZIARA MIRADI YA MKONGE TANGA

16 Aug, 2024
13:30:00 - 17:30:00
TANGA
PRO

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), ikiongozwa na Mwenyekiti wake Theobald Sabi, wamefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Mkonge mkoani Tanga ikiwamo mashamba na viwanda vya uchakataji Mkonge.

Lengo la ziara hiyo ni kujionea shughuli husika katika Sekta ya Mkonge na changamoto zinazowakabili wakulima na wote waliopo kwenye mnyororo mzima wa Sekta ndogo ya Mkonge.

Katika ziara hiyo, wajumbe hao wametembelea mashamba ya Hale na Magunga na viwanda vya uchakataji Mkonge.

 

WAKURUGENZI TSB WAFANYA ZIARA MIRADI YA MKONGE TANGA
Taasisi Shirikishi