'FURSA ZA WANAWAKE KWENYE MKONGE NI NYINGI'
'FURSA ZA WANAWAKE KWENYE MKONGE NI NYINGI'
Imewekwa: 14 Mar, 2025

Wanawake wametakiwa kuchangamkia fursa balimbali zilizopo katika Sekta ya Mkonge ili kujenga uchumi imara wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika Maonesho yanayoendelea kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Afisa Kilimo wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Jackline Mwashitete amesema Sekta ya Mkonge ina fursa nyingi kwa wanawake katika kilimo chenyewe cha Mkonge au bidhaa za Mkonge zinazozalishwa kwa mkono (handcraft).
"Sekta ya Mkonge ni mtambuka, kuna kilimo, biashara na fursa mbalimbali lakini wanawake wengi zaidi ya asilimia 35 wamejikita katika bidhaa za mkono kama vile ufumaji wa vikapu na urembo.
"Katika kuhakikisha tunaongeza uzalishaji kuhamasisha watu wengi zaidi kujikita kwenye kilimo cha Mkonge hususani wanawake. Pale Tanga tuna Kituo Atamizi kinatoa mafunzo mbalimbali ya kuzalisha bidhaa za Mkonge na wanawake ni miongoni mwa makundi yanayopewa kipaumbele," amesema.
Aidha, amebainisha mikakati ya TSB katika kuhakikisha inaongeza uzalishaji licha ya hamasa kwa wakulima lakini pia imeanza kufungua ofisi za Kanda ili kuwarahisishia wakulima wa Mkonge kupata huduma stahili kwa wakati na kwa ukaribu zaidi ambapo kwa sasa imefungua Kanda ya Magharibi ambayo Makao Makuu yake yako mkoani Tabora.
Matangazo ya hivi punde