TSB, TPA TANGA WAJADILI UTATUZI CHANGAMOTO USAFIRISHAJI MKONGE
TSB, TPA TANGA WAJADILI UTATUZI CHANGAMOTO USAFIRISHAJI MKONGE
Imewekwa: 25 Sep, 2025
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona amekutana na kufanya mazungumzo na Meneja wa Bandari ya Tanga, Saleh Mbega katika Ofisi za TSB jijini Tanga.
Katika mazungumzo yao walijadili mambo mbalimbali kuhusu ufanisi na changamoto za usafirishajiwa Mkonge kupitia Bandari ya Tanga na namna ya kuzitatua ili kuwezesha wakulima na wafanyabiashara wa Mkonge kutumia bandari hiyo.
Meneja Mbega ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Meneja katika bandari hiyo, aliongozana na ujumbe wake ambapo pamoja na mambo mengine alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa Mkurugenzi Kambona ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Taasisi za Serikali mkoani Tanga.








