UBUNIFU WA MASHINE WAFUNGUA NJIA YA KUONGEZA THAMANI YA MKONGE KISHAPU

Imewekwa: 27 Aug, 2026
UBUNIFU WA MASHINE WAFUNGUA NJIA YA KUONGEZA THAMANI YA MKONGE KISHAPU

Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) imefanya ziara katika Wilaya ya Kishapu, Mkoa wa Shinyanga kwa kutembelea eneo la mbunifu la mtengenezaji wa mashine mbalimbali zinazolenga kuongeza thamani ya zao la Mkonge.

Katika ziara hiyo, TSB imejionea ubunifu wa mashine za Raspado, Mobile Cleaner, Kayamba na Press, zilizobuniwa na kutengenezwa na Daud Magolyo kwa ajili ya kurahisisha shughuli za uchakataji na kuongeza thamani ya Mkonge.

Ziara hiyo imelenga kutambua na kuhamasisha ubunifu wa ndani unaoweza kuchangia kuongeza ufanisi katika uchakataji wa Mkonge, kupunguza changamoto za uzalishaji pamoja na kuongeza thamani ya bidhaa zitokanazo na zao hilo.

Bodi ya Mkonge Tanzania inaendelea kuhimiza matumizi ya teknolojia na ubunifu katika sekta ya Mkonge ili kuongeza tija na kukuza fursa za kiuchumi kwa wakulima na wadau wa sekta hiyo.

Taasisi Shirikishi
Hakimiliki ©2026 Bodi ya Mkonge Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa.