"Karibu katika Tovuti ya Bodi ya Mkonge Tanzania; Wewe ni wa thamani sana kwetu, asante kwa kutembelea tovuti yetu. Jiunge nasi ili ugundue singa asilia za Mkonge."
Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb), akipokea maelezo kuhusu maendeleo ya sekta ya Mkonge kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Bw. Saddy Kambona, alipotembelea Banda la Bodi katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika kwenye Viwanja vya Dkt. John Malecela, Nzuguni jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli, akipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) alipotembelea banda la Bodi katika Maonesho ya Nanenane, Viwanja vya John Samwel Malecela (Nzuguni), Dodoma.
Balozi wa Tanzania nchini China Dkt. Suleiman Haji Suleiman, akipata maelezo kutoka kwa maafisa wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotokana na Mkonge alipotembelea Banda la TSB katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Aristides Mbwasi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba)
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) Bw. Theobald Sabi akiongoza kikao cha Robo ya tatu ya Bodi kwa Mwaka wa fedha 2025/2026, Kilichofanyika katika Ofisi za TSB ( Mkonge House), jijini Tanga, tarehe 25 Juni 2026.
Shamba la Mkonge likiwa limepangwa kwa ustawi na uzalishaji endelevu.
Mashine ya kuchakata mkonge (dikotiketa) ni kifaa kinachotumika kuondoa nyama laini ya majani ya mkonge ili kubaki na nyuzi za mkonge zinazotumika kutengeneza kamba, mikeka, mazulia na bidhaa nyingine.
Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano umeshiriki katika Mkutano wa Dunia wa Kutokomeza Utumikishwaji wa watoto uliofanyika nchini Morocco. TSB imewakilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Emmanuel Kimaro ( wa tatu kulia)
Menejimenti ya Bodi ya Mkonge Tanzania yakutana na kuzungumza na timu ya tathmini kutoka ofisi ya Msajili wa Hazina na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) wakati wa kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa Bodi kiichofanyika Mkonge House jijini Tanga.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) Saddy Kambona akizungumza na timu ya tathmini kutoka ofisi ya Msajili wa Hazina na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) wakati wa kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa Bodi kiichofanyika Mkonge House jijini Tanga.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania ( TSB) Saddy Kambona (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula ( NFRA) Dkt. Andrew Komba katika kikao kazi cha Wakuu wa Taasisi za Kilimo kilichofanyika Jijini Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Dkt. Batilida Burian akifurahia elimu ya kilimo Mseto cha Mkonge aliyopata katika banda la Bodi ya Mkonge Tanzania( TSB) wakati wa ziara yake ya kutembelea mabada ya maonesho katika ufunguzi wa maonesho ya Wiki ya Chakula Duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Biashara wa Kampuni inayojihusisha na biashara ya matrekta nchini (TAFE), Praveen Makala na Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni hiyo, Bosco Raj.
Balozi wa Vietnam nchini Tanzania, Mhe. Vu Thanh Huyen ametembelea Ofisi za Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) jijini Tanga kwa lengo la kujifunza kuhusu mnyororo mzima wa thamani wa zao la Mkonge
Ziara ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TSB katika mradi wa Mruazi Heifer Breaeding Unit ( HBU)
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TSB wakagua mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kuchakata Mkonge cha Taula kilichopo wilaya ya Handeni Mkoani Tanga
Waziri wa Kilimo, Mh. Hussein Bashe (wa pili kulia), akionyeshwa maeneo mbalimbali ya ofisi za Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) wakati akienda kuzindua Kituo Atamizi cha Mkonge BBT Tanga kinachosimamiwa na TSB.
Waziri wa Kilimo, Mh. Hussein Bashe (kulia) akipokea zawadi ya picha ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan iliyozalishwa kwa zao la Mkonge sanjari na bidhaa nyingine zinazotokana na zao hilo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mh. Japhari Kubecha.